TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WASAIDIZI KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA UCHAGUZI MDOGO WA WADI YA NDAGONI WILAYA YA CHAKECHAKE PEMBA.

February 01, 2017  |   Latest News   |     |   0 Comment

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA ZIWANI ANATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA, WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA NA WAONGOZAJI WA WAPIGA KURA KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA UCHAGUZI MDOGO WA WADI YA NDAGONI.

MUOMBAJI WA NAFASI YA MSAIDIZI MSIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA NA MUONGOZAJI WA WAPIGA KURA ANATAKIWA AWE NA SIFA ZIFUATAZO.

I. AWE NI MZANZIBAR
II. AWE NI MKAAZI WA ENEO ANALOOMBA KUFANYA KAZI.
III. AWE NA ELIMU KWA KIWANGO CHA KIDATO CHA NNE NA KUENDELEA.
IV. AWE NA UWEZO WA KUFANYA SHUGHULI ZA UPIGISHAJI KURA.
V. AWE NA UZOEFU WA SHUGHULI ANAYOIOMBA NA,
VI. ASIWE NA USHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.

KWA MUOMBAJI WA NAFASI YA MSIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA ANATAKIWA AWE NA SIFA ZIFUATAZO.

I. AWE NI MZANZIBAR.
II. AWE NI MKAAZI WA ENEO ANALOOMBA KUFANYIA KAZI
III. AWE NA UMRI USIOPUNGUA MIAKA 30.
IV. AWE NA ELIMU KWA KIWANGO CHA KIDATO CHA NNE NA KUENDELEA AU UZOEFU WA KAZI YA USIMAMIZI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA USIOPUNGUA CHAGUZI MBILI.
V. AWE NA UZOEFU WA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
VI. AWE NA UWEZO WA KUFANYA DHAMANA ZAKE BILA KUSIMAMIWA.
VII. AWE NA UWEZO WA KUIFAHAMU JAMII YAKE ILIYOMZUNGUUKA
VIII. AWE NA UWEZO WA KUTEKELEZA SHERIA ZA UCHAGUZI
IX. AWE NA UWEZO WA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUFANYA HESABU KWA USAHIHI.
X. AWE NA UWEZO WA KUANDIKA RIPOTI. NA
XI. ASIWE NA USHABIKI WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.

MUOMBAJI WA NAFASI HIZO ATAWAJIBIKA KUAMBATANISHA NAKALA ZA VYETI VYA KUMALIZIA MASOMO KATIKA BARUA YAKE YA MAOMBI.
BARUA ZA MAOMBI ZITUMWE KWA ANUANI IFUATAYO.
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA ZIWANI.
P.O.BOX 1001,
ZANZIBAR

WAOMBAJI WOTE WANATAKIWA WAWASILISHE BARUA ZAO ZA MAOMBI KATIKA AFISI YA TUME YA UCHAGUZI YA WILAYA YA CHAKECHAKE PEMBA.
SIKU YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 5/02/2017 SAA ZA KAZI.

PIGA KURA KWA AMANI UPATE MAENDELEO NCHINI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR.

Related Posts

There is no related post.