ZEC IMETOA ELIMU KWA SHEHA NA WAJUMBE WAO.

February 08, 2017  |   Latest News   |     |   0 Comment

Jaala Makame Haji ZEC Zanzibar.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC ) imewataka masheha na wajumbe wao kuhakikisha wanaifanyia kazi elimu wanayopewa na Tume ya Uchaguzi ili kufikia malengo ya elimu hiyo ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ambazo hujitokeza katika kipindi cha uandikishaji na Uchaguzi.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa uandikishaji wa wilaya ya Kati Ndugu Mussa Ali Juma tarehe 7 Februari 2017 wakati alipokuwa akizungumza na masheha wa shehia ya Kidimni ikiwa ni muendelezo wa semina za masheha zinazotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa Shehia zote za Unguja na Pemba.

Akizungumza katika semina ya sheha na wajumbe wa shehia ya Chutama iliyofanyika Wilaya ya Kaskazin “A’  ,   sheha wa shehia hiyo Ndugu Iddi Ali Fumu alisema, shehia yake imejipanga vizuri kuhakikisha wanashirikiana na Tume kuitumia Vizuri elimu waliyoipata kwani elimu hiyo imewafumbua macho wakati hapo kabla walikuwa hawana elimu yeyote juu ya masuala ya kiuchaguzi.

Naye Sheha wa Shehia ya Mwera Bw. Khamis Bilali Risasi aliwaasa masheha wa Zanzibar kutilia mkazo wananchi wanaohamia katika maeneo yao kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizowekwa na serikali ili kuondoa migogangano na mifarakano katika jamii hasa wakati wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

DSC04816

Sheha wa Shehia ya Mwera kushoto Ndg Khamis Bilali Risasi kwa makini akisikiliza maelezo katika semina iliyofanyika Skuli ya Mwanakwerekwe “C” tarehe 7 Februari 2017, semina ambayo ilitolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( picha na Jaala Makame Idara ya habari ZEC)

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC mara baada ya Semina ya masheha wa Fuoni Kibondeni na Masheha wa Mwera, Afisa Uandikisha Tume ya Uchaguzi ZEC Ndugu Amour Ameir Hafidh alisema ZEC itaendelea kutoa Elimu ya Wapiga Kura kwa Wadau wengine wa Uchaguzi wakiwemo watu wenye mahitaji maalum.

Wakati akiwasilisha mada katika semina hiyo Afisa uandikishaji Wilaya ya Magharib “A” Ndugu Ali Rashid Suluh aliwaasa masheha wa Unguja na Pemba ambao wao ni wakala wa Uandikishaji kuzingatia sifa za wananchi wao wakati wanapokwenda vituoni kwa ajili ya kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Kupiga Kura ikiwa ni pamoja na sifa ya ukaazi wa eneo husika.

DSC04812

Afisa uandikisha wilaya ya Magharib A akiwafahamisha masheha wa shehia ya Fuaoni Kibondeni na shehia ya Mwera kuhusu masuala ya uendelezaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika semina iliyofanyika tarehe 7 Februari,2017 skuli ya Mwanakwerekwe “C” Mjini  Unguja ( kulia ni Afisa Uandikishaji ZEC Ndg Amour A. Hafidh na Kushoto ni Ms. Afisa Uandikishaji Wilaya ya Kaskazin “B”)( picha na  Idara ya habari ZEC)

Afisa huyo alifahamisha kuwa, ili mtu andikishwe katika Daftari la kudumu la wapiga kura ni lazima awe mzanzibar, atimie miaka kumi na nane na awe mkaazi wa eneo husika analoomba kuandikishwa .

Aidha, Ndugu Ali Suluhu aliwasihi masheha kuwamakini zaidi na sifa ya ukaazi kwa watu ambao wanahamia katika eneo hilo ni lazima watimie miezi thelathini na sita (miaka Mitatu) lakini kunawatu waliotajwa katika Sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya 1984 ambao ni wategemezi, waliohamia kikazi na wanandoa nao wanapaswa kuzingatiwa zaidi.

Semina za masheha zinaendelea kutolewa na Tume ya Uchaguzi kwa Unguja na Pemba ambazo hutolewa kila mwezi mara nne kwa wilaya zote 11ambapo jumla ya shehia 44 kila mwezi hufaidika na semina hizo.
Kwa mwezi wa Februari 2017 semina hizo zitafanyika tarehe 7, 14, 21 na 28,kwa wilaya zote za Unguja na Pemba

Related Posts

There is no related post.