ZEC. ELIMU YA WAPIGA KURA NI ENDELEVU

February 27, 2017  |   Latest News   |     |   0 Comment

Jaala  Makame  Haji  ZEC

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inajukumu la kuratibu na kusimamia shughuli za elimu ya wapiga kura kwa mujibu wa kifungu cha 5(b) cha sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya 1984 iliyotungwa na Baraza la wawakilishi la Zanzibar mwaka 1984 yenye nia ya kuweka utaratibu mzuri wa kupiga kura ambayo matlaba yake ni kuwachagua viongozi kwa njia ya kidemokrasia.

Katika utekelezaji mzuri wa jukumu hilo la utoaji wa elimu ya wapia kura,Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya kila linalowezekana kuhakikisha inatumia njia mbali mbali za kuweza kuwafikia  kwa haraka zaidi wadau wa Uchaguzi, pale Tume inapohitaji kutoa taarifa au elimu juu ya masuala ya kiuchaguzi.

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imeandaa mpango endelevu wa utoaji elimu  ya wapiga kura ili kuboresha uhusiano wa karibu wa kupeana taarifa baina ya Tume na wadau wake ambapo ni tofauti ilivyozoeleka, hapo kabla Tume ilikuwwa inatoa elimu ya wapiga kura kila inapofika kipindi cha maandalizi ya  uandikishaji na Uchaguzi tu.

Wakati akifungua semina ya Masheha wilaya ya Magharib A na B iliyofanyika tarehe 17 Januari 2017 katika ukumbi wa skuli ya Mwanakwerekwe “C” Afisa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndugu IDRISA HAJI JECHA alisema mpango wa elimu endelevu umeandaliwa makusudi kuondoha changamoto zilokuepo na kuboreha uhuiano ili kupanua wigo wa kukusanya taarifa kutoka kwa wadau wa Uchaguzi wakiwemo Masheha ikiwemo taarifa za watu waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari la Kudumu la wapiga kura.

Afisa Idrisa  alisema, katika kuimarisha utendaji wake Tume imejiandaa vya kutosha kuhakikisha kila baada ya miezi mitatu inaendesha zoezi la kuwafuta watu waliokosa sifa za kuwemo katika daftari la wapiga kura ambapo ni tofauti na miaka iliyopita kwani zoezi hilo lilikuwa likifanywa kila baada ya miezi sita.

Katika Mpango wa utekelezaji wa elimu endelevu ya wapiga kura, Tume imepanga kukutana na masheha wote wa Unguja na Pemba kwa kuwafanyia semina maalum juu ya utaratibu wa uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Kwani kufanya hivyo kutarahisisha uelewa mzuri kwa masheha juu ya ukusanyaji wa taarifa za wapiga kura katika shehia zao.

Ndugu Idrisa aliendelea kusema, Tume bado inaamini kuwa mtu yeyote anayeandikishwa kuwa mpiga kura bado anakuwa chini ya dhamana ya sheha wake mpaka anapopoteza sifa za kuwa mpiga kura na ndio maana ZEC inashirikiana kwa karibu na masheha katika kutekeleza majukumu ya kiuchaguzi ikiwemo Uandikishaji wa wapiga kura na uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwani bila uwepo wa masheha kazi hizo haziwezi kutekelezwa kwa ufanisi mzuri.

Sheha anajukumu la kumtambua mwananchi ikiwa anazosifa au hanasifa za kuandikishwa katika eneo lake la kiuchaguzi, lakini pia mwananchi huyo baada ya kuandikishwa atakuwa chini ya uangalizi wa sheha wake kwa kuwa bado sheha  atawajibika kumpatia huduma mwananchi huyo wakati akihitaji kupata shahada nyengine wakati atakapopoteza shahada yake,kuhamisha taarifa au kufanya marekebisho ya taarifa zake katika daftari la wapiga kura na mwisho sheha atawajibika kutoa taarifa Tume pindipo mwananchi atapoteza sifa za kuwemo katika daftari la kudumu

Inaelezwa kwamba, mtu anaweza kupoteza sifa za kuwemo katika Daftari la kudumu la wapiga kura, iwapo moja kati ya sifa zifuatazo atakuwanazo ambazo ni pamoja na kufariki, kuukana uraia na kuwa na uraia wa nchi nyengine.

Ndugu Idrisa alisisitiza kwa kusema kwamba, kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi Nam.11 ya mwaka 1984 kifungu cha 11A(2)(3) inamtambua sheha kuwa ni mdau muhimu wa Tume wakati wa uandikishaji wa wapiga kura wapya na uendelezaji wa daftari la kudumu la  wapiga kura  kutokana na wadhifa wake anakuwa ni wakala wa uandikishaji wa Tume katika shehia ambayo yeye ni sheha.

Sambamba na hayo, Kwa upande wa ukusanyaji wa taarifa za wapiga kura waliokosa sifa, ofisi za wilaya kwa kushirikiana na masheha zimekusanya jumla ya taarifa za wapiga kura 6,743 kati ya hao wapiga kura 2,765 ni wanawake na wanaume ni 6,978.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa uchaguzi Ndugu Salum Kassim Ali tarehe 29 Disemba 2016 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi,ilibainisha kwamba, orodha za wapiga kura hao zilibandikwa sehemu za wazi nje ya ofisi za Tume za Wilaya na ofisi za Masheha kuanzia tarehe 5 Disemba hadi 11 Disemba 2016 kwa lengo la kupokea maoni na malalamiko ya wapiga kura dhidi ya orodha hizo.

Katika taarifa yake Ndugu Salum Kassim alisema, kufuatia kukamilika kwa hatua hiyo ya kubandika orodha za wapiga waliokosa sifa, Tume itawafuta wapiga kura hao kutoka katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Aidha,akizungumza katika semina ya masheha wa Moga na Gamba wilaya ya kaskazini “A” ikiwa ni utekelezaji wa mpango enedelevu wa utoaji wa elimu ya wapiga kura Afisa elimu ya wapiga kura Ndugu Juma Sanif Sheha aliwaomba masheha kuendelea kufanya kazi kwa mashirikiano na wajumbe waopamoja na  Tume wakati wakukusanya taarifa za wapiga kura waliokosa sifa za kuwemo katika Daftari la kudumu la wapiga kura.

tutakuwa mashahidi juzi tu tulipobandika orodha za watu waliopoteza sifa, haya yote yanaonesha kuwa shughuli hii haikufanywa na Tume peke yao bali na sheha pamoja na wajumbe wake”  ni kauli ya Ndugu Juma Sanifu alipokuwa akizungumza na masheha wa shehia ya Gamba na Moga katika semina iliyofanyika tarehe 17 Januari 2017 Afisi za Tume za Wilaya Kaskazini “A”

Kwa hili la Kutoa taarifa kuhusu watu waliopoteza sifa na taarifa nyengine yeyete ile yenye makusudi ya kujenga taifa letu ni wajibu wa kila mwananchi katika maisha yake ya kila siku na sioo lazima mwananchi afuatwe na sheha wake kwani  huo ndio ushrikiano unaozungumzwa na viongozi wetu.

DSC04967

Afisa Elimu ya Wapiga Kura Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndg. Juma Sanifu Sheha kulia ni Afisa Uandikishaji Wilaya ya Magharib “B” Ndg. Khamis Mussa na Kushoto ni Afisa uandikishaji Wilaya ya Magharib “A’ Ndg. Ali Rashid Suluhu wakiwa katika Semina za Masheha zinazoendelea kutolewa na Tume kwa Wilaya zote za Unguja Na Pemba. (Picha na Jaala Makame ZEC)

Aidha, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imekuwa ikipiga kelele kwa wapiga kura ambao wanahitaji kufanya marekebisho ya taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura kwenda katika Afisi za Wilaya za Tume kwani wengi wao husubiri kipindi cha Uchaguzi kitendo ambacho husababisha foleni kubwa katika Afisi hizo.

Afisa uandikishaji wilaya ya Kaskazini “A” Ndugu Bakari Burhan aliwasihi masheha kuwaongoza wananchi wao katika kufuata taratibu ambazo zinawekwa na Tume ya Uchaguzi ZEC juu ya huduma za Uendelezaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwemo utaratibu wa kupatiwa shahada mpya kwa wale waliopoteza au kuharibika shahada zao na utaratibu wa kuhamisha taarifa kutoka eneo moja la Uchaguzi na kwenda eneo jengine.

Akizungumza na masheha na wajumbe wa shehia ya Karakana na Chumbuni katika ukumbi wa Afisi ya Tume tarehe 223 Feb,2017 , Ms. Afisa unadikishaji Wilaya ya Mjini Ndugu mohamedi Ali Abdallah aliwaasa masheha hao kutoa taarifa sahihi za watu wanaotapaswa kufutwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili kuepusha migongano ya kiuchaguzi isiyokuwa ya lazima.

Kwa nyakati tofauti,wakizungumza kuhusu suala la kuhama na kuhamia katika makazi mapya sheha wa shehia ya Mkataleni wilaya ya Kaskazini “B’ Ndugu Sharif Ali, Mjumbe wa shehia hiyo Bibi Mantanga Bakari na wajumbe wa Sheha wa shehia ya ChaChani wilaya ya Chakechake waliaasa wananchi kwamba ni vyema kufuata taratibu zilizowekwa na serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Sheha wakati wa kuhama na kuhamia katika makazi mapya ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.

Wakati mwengine mizozo ya uandikishaji hutokea kwa kutokuwepo kwa majina ya mitaa hivyo, mamlaka inayohusika ikiwemo Baraza la mji  kuweka majina ya mitaa hasa ile mitaa mipya ipewe majina ili itambulikane kwani baraza  hilo limepewa mamlaka ya kutangaza majina ya mitaa katika Gazeti Rasmi la Serikali, kauli hiyo ilitolewa na wajumbe wa Shehia ya ChaChani katika semina  iliyofanyika tarehe 19 Januari 2017 ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Mpango endelevu wa utoaji wa elimu ya Wapiga Kura

Afisa uandikihaji kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bw. Amour Ameir Hafidh Aliwaomba Masheha hao kwamba, ni vyema kuifikisha kwa wananchi elimu wanayopatiwa  ili kuondoa mivutano ambayo hujitokeza kipindi cha Uchaguzi kwani Tume inafanya jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa wadau wake kwa madhumuni ya kuondoa changamoto za kiuchaguzi.

Masheha hao walikiri kwamba kabla ya semina hizo hawakuwa na uelewa mkubwa juu masuala haya ya Uendelezaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na masuala ya Uandikishaji wa wapiga kura wapya na kuiomba Tume iendelee zaidi kutoa elimu hasa kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya kisiasa katika visiwa vya Zanzibar.

Mpaka kumalizika kwa mwezi wa Juni,2017 Jumla ya Shehia 528 wakiwemo masheha na wajumbe wao wa Unguja na Pemba wawetayari wamefaidika na elimu inayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, sambamba na vipindi 24 vya redio vya kurikodiwa vitakua tayari vimerushwa na Tume ya Uchaguzi ZEC kupitia shirika la utangazaji la Zanzibar ( ZBC ).

Related Posts

There is no related post.