ZEC. VIJANA SOMENI HISTORIA YA NCHI YENU.

April 13, 2017  |   Latest News   |     |   0 Comment

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar inatarajia kuandikisha Wapiga Kura Wapya ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo vijana walitakiwa kujiandaa kwa ajili ya kuandikishwa kwa kutafuta vitambulisho vya uzanzibari ukaazi kwa wale ambao hawajapata vitambulisho hivyo.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar Mh. Jecha Salim Jecha aliwaomba viongozi wa Mabaraza ya vijana nchini na jumuiya nyengine za Vijana kukaa na kujadili namna ambavyo watafikisha taalama ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la Kudumu la kupiga kura kwa wale vijana ambao wamefikia umri wa kuandikshwa na ambao bado hawaja andikshwa,

Mwenyekiti Jecha aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua semina ya makundi ya Vijana tarehe 12 Aprili, 2017 katika ukumbi wa Elimu Mbadala Raha leo Mjini Zanzibar, semina hiyo iliandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa lengo la kutoa elimu juu ya masuala ya uandikishaji na uendelezaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

DSC05201

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mh. Jecha Salim Jecha akifungua Semina ya Makundi ya Vijana katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Raha leo Mjini Unguja. tarehe 13.4.2017.

Aidha, Mh. Jecha aliongeza kwa kusema imefika muda sasa hivi kwa vijana kujua umuhimu wa kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi na ni lazima kuwa na uchungu wan chi zao kwa kusoma historia ya nchi ili wajuwe wapi wanatoka, wapi walipo na wapi wanakoenda.

Hata hivyo. Aliwaonya baadhi ya wanachama wa siasa wanaoshawishi wananchi kwa katika taasisi za kidini kwa kununua Shahada za kupigia kura za wanachama wa chama chengine kwa maslahi yao ya kisiasa, alisema changamoto hii ilijitokeza zaidi katika Uchaguzi uliopita wa mwaka 2015.

Akiwasilisha mada ya nafasi za Vijana katika kujiletea maendeleo Ndugu, Shaib Ibrahim Muhammed aliwaomba wadau wa maendeleo kuanzisha programm maalum zitakazo yawezesha mabaraza ya vijana Zanzibar kujiletea maendeleo yao binafsi.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana taifa Ndugu. Khamis Rashidi (MAKOTI) aliiomba Tume kuandaa program maalum ya kupita katika kila Wilaya ili kutoa elimu kwa wajumbe wa Mabaraza ya Vijana Wilaya. Sambamba na kuwaomba vijana waungane na Tume ya Uchaguzi na taasisi nyengine kutoa taaluma inayohusiana na mambo ya kidemokrasia.

DSC05267

mshiriki wa semina ya makundi ya Vijana kutoka katika jumuiya ya The Voice of the Voiceless Foundation. Bibi. ANATOLIA G. KASIRA.

Wakati wakichangia mada katika semina hiyo, washiriki wa semina hiyo wameishukuru tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kuandaa semina za kutoa elimu kabla ya kipindi cha Uchaguzi jambo ambalo litaweza kuondoa changamoto nyingi ikiwemo ya kupunguza vurugu zisizokuwa za lazima.

Related Posts

There is no related post.