WATENDAJI WA AFISI YA ZEC WAPATIWA MAFUNZO YA KIUTUMISHI

April 11, 2018  |   Latest News   |     |   0 Comment

Jaala Makame Haji

ZEC- Zanzibar

Watendaji wa Afisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar wametakiwa kufuata maelekezo na taratibu zote zilizowekwa na Sheria ya Utumishi wa Umma Nam. 2 ya 2011 pamoja na kanuni zake za mwaka 2014 ikiwa pamoja na kutii maagizo wanayopewa na waajiri wao.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa kurugenzi ya Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndugu IDRISSA HAJI JECHA katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi ya Tume Wilaya ya Mjini tarehe 05 Aprili, 20018 alipokuwa akifunga mafunzo ya siku moja ya Sheria ya Utumishi wa Umma Nam.2 ya 2011 na kanuni zake za mwaka 2014.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Afisi ya Tume ya Uchaguzi na kuwa shirikisha Watendaji wote wa Afisi hiyo upande wa Unguja kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji kwa Watendaji wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku .

Akiwasilisha mada ya Wajibu na Haki za watumishi wa Umma Afisa Mipango wa Tume ya Uchaguzi Bi LUTFIA FAIDA HAJI alisema mfanyakazi anapaswa kuipenda kazi yake kwa bidii, kupenda kujifunza, kujielimisha na kujiendeleza pamoja na kufuata taratibu zote za kazi na kuitumia vyema elimu aliyoipata kama zilivyoelekeza kanuni za maadili.

Afisa Mipango Kutoka Afisi ya Tume ya Uchjaguzi ya Zanzibar BI LUTFIA FAIDA HAJI akiwasilisha mada katika mafunzo ya Watendaji wa Afisi hiyo, yalifanyika katika ukumbi wa mikutano Afisi ya Tume Wilaya ya Mjini tare he 05 Aprili, 2018

(Afisa Mipango Kutoka Afisi ya Tume ya Uchjaguzi ya Zanzibar BI LUTFIA FAIDA HAJI akiwasilisha mada katika mafunzo ya Watendaji wa Afisi hiyo, yalifanyika katika ukumbi wa mikutano Afisi ya Tume Wilaya ya Mjini tare he 05 Aprili, 2018)

Wakati akihitimisha mada yake BI LUTFIA aliwanasihi wafanyakazi kwa kusema kwamba, Utoaji wa huduma lazima uwe sawa, huru, haki na bila ya upendeleo na uimarishe matumizi bora na sahihi ya rasilimali

Aidha, Afisa Mipango Bi Lutfia aliendelea kwa kusema kwamba, Utumishi wa Umma lazima ukidhi misingi ya uwajibikaji, mahitaji ya watu ni lazima yatimizwe na watu washajihishwe kushiriki katika utungaji wa sera.

Nao washiriki wa mafunzo hayo waliushukuru Uongozi wa Afisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatakuwa ni muongozo kwao wakati wa kutekeleza kazi zao.

Afisa Mipango Kutoka Afisi ya Tume ya Uchjaguzi ya Zanzibar BI LUTFIA FAIDA HAJI akiwasilisha mada katika mafunzo ya Watendaji wa Afisi hiyo, yalifanyika katika ukumbi wa mikutano Afisi ya Tume Wilaya ya Mjini tare he 05 Aprili, 2018

Watendaji wa Afisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar wakiwa katika Mafunzo ya siku moja kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika tarehe 05 Aprili,2018 katika ukumbi wa Tume Wilaya ya Mjini

Hata hivyo, watendaji hao wa Afisi ya Tume wameuomba Uongozi wa Afisi yao kuandaa mafunzo mengine mara kwa mara kwa lengo la kuongeza utendaji kazi wao kiufanisi.

mada zote zilizosomeshwa katika mafunzo hayo ziliwasilishwa na Maafisa kutoka Tume ya Uchaguzi ambazo ni pamoja na Sheria ya Utumishi wa Umma Nam. 2, 2011 iliyowasilishwa na kaimu Mkuu wa Kitengo cha sheria Ndg Mbaraka Said Hassuni, mada ya maadili ya Watumishi wa Umma iliyosilishwa na Msaidizi Afisa Utumishi Bi Shadya MwinyiUssi Khatibu, mada ya Wajibu na Haki za Wafanyakazi iliwasilishwa na Afisa Mipango BI Lutfia Faida Haji na Afisa Habari na Uhusiano Ndugu Jaala Makame Haji aliwasilisha Mada ya Utawala Bora.

Related Posts

There is no related post.