MAENEO NA KITUO CHA KUPIGIA KURA

Katiba ya Zanzibar imeipa mamlaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendesha Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano na Uchaguzi Mdogo wa kujaza viti vilivyoachwa wazi katika ngazi ya Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Hata hivyo, ili Tume iweze kuendesha uchaguzi kwa ufanisi mkubwa huandaa utaratibu wa kuligawanya kila jimbo la uchaguzi katika maeneo ya uchaguzi  ili kuwawezesha wapiga kura wa eneo husika la uchaguzi kupiga kura kwa urahisi bila ya kuifuata huduma hiyo katika masafa marefu. Aidha, kwa ajili ya kurahisisha upigishaji wa kura kila eneo la uchaguzi hugawanywa katika vituo vya kupigia kura.

Idadi ya maeneo ya uchaguzi na vituo vyake hutegemea ukubwa wa jimbo husika, mkato wa mipaka ya utawala na idadi ya wapiga kura wanaotarajiwa kupiga kura katika jimbo husika. Maeneo ya kupigia kura katika majimbo mengi ya uchaguzi yamo katika majengo ya umma kama vile skuli, kumbi za kijamii au Ofisi za  Mamlaka za Serikali za Mitaa. Ifuatayo ni orodha ya maeneo ya kupigia kura na vituo vyake Kimkoa, Kiwilaya na Kijimbo.

Orodha hiyo, inabadilika kutoka uchaguzi mmoja na mwengine kutokana na mabadiliko ya mipaka ya majimbo, mabadiliko ya mipaka ya utawala ambayo mara nyingi hupelekea ongezeko au kupungua maeneo hayo kutoka jimbo moja kwenda jengine.

Bofya hapa kupata orodha ya vituo vya kujiandikisha.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii