Na Jaala Makame Haji - ZEC

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imekabidhi kwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi ripoti ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar uliofanyika Oktoba 28, 2020. Akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar Raisi wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alisema Serikali yake inaahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote zilizoelezwa katika Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 ili kuzifanya chaguzi zijazo kufanyika kwa ufanisi mzuri Zaidi Dk. Mwinyi alifafanua kuwa, chaguzi zijazo zitakuwa huru Zaidi kutokana na Tume ya Uchaguzi kufanikiwa kuwa na Miundo ya kisasa ambayo yanaifanya Tume hiyo kuenda na wakati.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe. Jaji Mkuu (Mst) HAMID MAHMOUD HAMID (kushoto) akimkabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2020 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi (kulia) tarehe 13 Julai, 2021 Ikulu Jijini Zanzibar 

Hata hivyo, Raisi wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi aliishukuru Tume pamoja na wote waliohusika kuendesha Uchaguzi Mkuu ambapo aliipongeza Tume kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu kwa mafanikio makubwa Zaidi ikiwa pamoja na kutoa matokeo ya Uchaguzi huo katika muda uliopangwa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akionesha ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2020 mara baada ya kupokea ripoti hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe. Hamid Mahmoud Hamid tarehe 13 Julai, 2021.

Mapema akiwasilisha ripoti hiyo Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 27 cha Sheria ya Kuanzishwa Afisi ya Tume ya Uchaguzi Namba 1 ya mwaka 2017 Tume inatakiwa kutayarisha Ripoti na kuiwasilisha kwa Muheshimiwa Rais ndani ya miezi 12 Mheshimiwa Hamid alifafanua kuwa ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa 2020 iliyowasilishwa kwa Mheshiwa Raisi wa Zanzibar imezingatia hali ya kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii