Vyama sita vya Siasa Visiwani Zanzibar vimejitokeza katika zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uteuzi wa Wagombea kwa Uchaguzi Mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe kwa Pemba na Udiwani kwa Wadi ya Welezo Unguja   katika kuwania nafasi hizo katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba  2023.

Vyama  vilivyojitokeza  kuchukua fomu za Uteuzi hadi sasa kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kwa Wadi ya Welezo Unguja ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo atakaewania ni Ndugu.Abdul-rahman H. Shaaban na Ndugu.Omar S. Dafa wa Chama cha Demokrasia Makini na Ndugu.Mohammed R. Vuai wa Chama cha UPDP

 Na kwa upande wa Uwakilishi kwa Uchaguzi Mdogo wa Mtambwe Pemba ni Ndugu.Mohammed Ali Suleiman wa Chama cha ACT Wazalendo na Ndugu.Hamad Khamis Hamad wa Chama cha Mapinduzi  (CCM)  na Ndugu.Mohammed Masoud Rashid wa Chama cha CHAUMA.

Kwa upande wa Unguja Wagombea wa Uchaguzi huo wamekabidhiwa fomu za Uteuzi na Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Magharibi ‘A’ Bi.Mwanapili  Kh. Mohammed  na  kwa upande wa Pemba Fomu za Uteuzi zimekabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Wete Ndugu.Othman Khamis Othman.

Kwa Uchaguzi Mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe  Fomu za Uteuzi kwa wagombea zimeanza kutolewa  tarehe 01 Oktoba,2023 hadi tarehe 07,Oktoba 2023 na kwa Uchaguzi Mdogo wa Wadi ya Welezo uchukuaji na urejeshaji wa Fomu umeanza tarehe 02 Oktoba,2023 hadi tarehe 08 Oktoba,2023.

Akizungumza  kwa niaba ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) baada ya kukabidhi fomu hizo Afisa Uchaguzi Msaidizi wa Wadi ya Welezo Bi.Mwanapili Khamis  Mohammed  kwa wagombea  hao wa nafasi ya Udiwani amesema, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC) imeshamaliza maandilizi yote  ya Uchaguzi huo na sasa zimebaki taratibu chache tu ambazo zipo katika ratiba za Uchaguzi mdogo ikiwemo zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa Fomu za Uteuzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Uchaguzi Mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe na Udiwani kwa Wadi ya Welezo unatarajia kufanyika tarehe 28,Oktoba 2023.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii