Mkuu wa Kurugenzi wa Huduma ya Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndugu.Khamis Issa Khamis amewataka Wasaidizi Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura Uchaguzi Mdogo wa Wadi ya Welezo kuzingatia mafunzo na kufuata  miongozo ya Kisheria ili kuepusha  kuvuruga Uchaguzi huo.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mdogo wa Wadi ya Welezo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi huo kabla ya zoezi la Kupiga Kura.

Amesema Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wanapaswa kufuata na kuzingatia miongozo ya kisheria kulingana na kile ambacho wataelimishwa na wanapaswa kuyafanyia kazi kwa utaratibu uleule watakaoelekezwa na kwa kuzingatia uaminifu,uadilifu na kujiamini.

Amesema utaratibu wa Uchaguzi si jambo rahisi na ni vyema Wasimamizi Wasaidizi kujiandaa vya kutosha na kuepuka kufanya makosa kwani wao ndio wanapaswa kufanya kazi kwa umakini,na ni vyema kuzingatia sifa zilizotolewa na Tume ikiwemo kutokuwa shabiki wa Chama cha Siasa kwani Wasaidizi Wasimamizi ni sehemu ya waendeshaji wa zoezi zima la Uchaguzi hivyo haipaswi kushabikia Chama chochote cha Siasa.

Akizungumzia baadhi ya changamoto wanazokutana nazo kwa baadhi ya Wasimamizi Wasaidizi hasa  Wasimamizi wa Vituo,

Amesema “kwa muda mrefu sasa kumekukuwa na changamoto kwa baadhi ya watu wanaopata nafasi ya usimamizi wa Kituo hasa katika ujazaji wa fomu za matokeo hivyo ni vyema kwa wale ambao watapewa nafasi hiyo kuongeza umakini katika suala hilo”

Kwa upande wake msaidizi msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la welezo Mwanapili Khamis Muhammed amewashauri wasimamizi wa vituo

vya kupigia kura kuwa makini katika matumizi na ujazaji wa fomu na kuingiza katika bahasha za kuhifadhia kura kwa usahihi ili kuepusha makosa.

Akiwasilisha mada kuhusiana na majukumu ya wasimamizi wa vituo vya Wapiga Kura Msaidizi Afisa uchaguzi wilaya ya Kaskazini ‘’ A’ ndugu.Jaala Makame Haji amesema ni muhimu kwa wasimamizi wa vituo kufuata sheria ,miongozo ,kanuni pamoja na busara ili kuhakikisha wanatekeleza majukuku yao ya msingi kwa uweledi

Uchaguzi Mdogo wa  Wadi ya Welezo  unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba 2023 na unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Wadi hiyo.

Mawasiliano Yetu

Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii