Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar   imewataka Maafisa Uandikishaji wa Wilaya kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo itatumika katika zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura Wapya kwa 2023.

Wito huo ulitolewa na Kamishna wa Tume hiyo Mheshimiwa Juma Haji Ussi wakati akifungua mafunzo kwa maafisa Uandikishaji wa Wilaya zote za Unguja na Pemba yaliyofanyika katika Afisi za Tume Maisara Mjini Zanzibar.

Mheshimiwa Juma alisema, Shughuli za Uandikishaji ni shughuli endelevu ambapo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hutengeneza miongozo mbalimbali ya Kisheria hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kuchukua hatua stahiki katika zoezi hilo ili hudumazitakazotolewaziinufaishejamii.

Kwa   upande mwengine aliwataka Waandishi wa habari kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar katika kutoa elimu kwa Wananchi ambao bado hawajaandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura juu ya umuhimu wakujiandikisha kuwa Wapiga Kura.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina aliwasisitiza Wananchi ambao wana sifa za kuandikishwa kujitokeza kwa wingi kuomba kuandikishwa kuwa wapiga kura na kuahidi kuwa Tume, itamuandikisha kila Mwananchi ambaye atafika kituo nikuomba kuandikishwakatikaDaftari la Kuduma la Wapiga Kura.

Akiwasilisha mada Mkuu wakurugenzi ya Huduma za Uchaguzi kutoka Tume ya Uchaguzi Khamis Issa Khamis aliwaomba Maafisa Uandikishaji kuwaeleza Makarani Uandikishaji kuwapa kipaumbele Watu wenye mahitaji maalum wanapofika vituoni kwa mujibu wa maelekezo ya sera Jinsia na ushirikishwaji wa Makundi ya Kijamii ya mwaka 2015 iliyoaandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Ndugu Khamis aliongeza kwa kusema kuwa karani wa Uandikishaji anawajibu wa kufuata miongozo ya kisheria na kanuni wakati akitekeleza majukumu yake katika kituo cha kujiandikisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Kurugenzi ya Mipango, utumishi na Utawala Saadun Ahmed Khamis wakati akiwasilisha mada ya kanuni za maadili na utaratibu wa mawasiliano aliwataka Watendaji wa Tume ya Uchaguzi kutotoa siri za taasisi wakati na baada ya kumaliza utumishi wao ndani ya Tume.

Nao washiriki wa Mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambapo wameahidi kuyazingatia mafundisho waliyopatiwa ili kufanikisha zoezi la Uandikishaji wa Wapiga kura wapya.

Mafunzo ya Maafisa wa Uandikishaji Wilaya yalifanyika ikiwa ni maandalizi ya Uandikishaji wa Wapiga Kura Wapya unaotarajiwa kuanza tarehe 2 Disemba 2023 katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii