Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  imemaliza zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura Wapya kwa awamu ya kwanza na inatarajia kufanya zoezi la Uandikishaji kwa awamu ya pili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa kutembelea vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Jaji George J. Kazi “zoezi la Uandikishaji kiujumla limekwenda vizuri na hakuna changamoto yoyote iliyosababisha kuzuia zoezi hili kwa njia moja au nyengine” alisema

Sambamba na hilo amewashukuru wadau wa Uchaguzi kwa ujumla wakiwemo  wananchi waliojitokeza,asasi za kiraia,vyombo vya Habari na shukurani za kipekee alitoa kwa Vyama vya Siasa kwa utulivu na mashirikiano yao wakati wa zoezi  hilo, amewashukuru Mawakala wenye uwakilishi kwa Vyama vyao waliojitokeza katika zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Shehia mbali mbali pamoja na kuwahamasisha wananchi katika kampeni ya  kujitokeza katika zoezi hilo.

Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura kwa Awamu ya kwanza lilianza rasmi tarehe 02 Disemba 2023 na limetamatika katika Wilaya ya Mjini tarehe 15 Januari 2024.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii