UCHAGUZI MDOGO

Uchaguzi Mdogo kwa Zanzibar, hufanywa na Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kujaza kiti kilichoachwa wazi na mtu aliyekuwa anashikilia kiti hicho katika Serikali Kuu, Baraza la Wawakilishi au katika moja ya vyombo vya Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Baraza la Manispaa, Baraza la Mji au katika Halmashauri ya Wilaya). Sababu zinazopelekea kuwepo na Uchaguzi Mdogo zimeainishwa katika Katiba na Sheria inayosimamia Uchaguzi. Katiba ya Zanzibar katika vifungu vya 34(1) na 71 imeelezea sababu zinazopelekea kufanyika Uchaguzi Mdogo kisheria. Vile vile, Sheria ya Uchaguzi, Na.4, 2018, kifungu cha 40(1) imeainisha aina tatu za Uchaguzi Mdogo zinazoendeshwa na Tume ili kujaza kiti kilichoachwa wazi cha Rais wa Zanzibar, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mjumbe katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Diwani).  Chaguzi hizo  na sababu za kufanyika kwake kama ifuatavyo:-

  • Uchaguzi Mdogo wa Rais

Uchaguzi Mdogo wa Rais, unafanyika kwa mujibu wa masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 34 cha Katiba ambacho kinaeleza kuwa, “endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kwa sababu ya kufariki au kujiuzulu au kwa maradhi chini ya kifungu cha 33 cha Katiba hii, nafasi hiyo itajazwa kama ifuatavyo:

(i) iwapo Rais aliyekuwepo ametumikia kwa muda wa chini ya miaka minne, basi mtu anayefuatia kwa madaraka kwa mujibu wa kifungu cha 33(1) cha Katiba atachukua madaraka ya Urais kwa muda na uchaguzi utaitishwa ndani ya siku mia moja na ishirini, na uchaguzi huo utaendeshwa kwa utaratibu ulioelezwa katika vijifungu vya (2) hadi (7) vya kifungu hiki”.  Uchaguzi Mdogo wa Rais kufanyika Zanzibar katika mwaka 1984 wakati aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo Mhe. Aboud Jumbe Mwinyi alipojiuzulu katika kiti hicho na tarehe 19 Aprili mwaka 1984 ulifanyika uchaguzi wa kuziba kiti kilichoachwa wazi ambapo, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alichaguliwa kuwa Rais wa tatu wa Zanzibar katika uchaguzi mdogo huo.

Bofya hapa kupata maelezo zaidi

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii