Na Ahmed A. Mohammed = ZEC

Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wamekumbushwa kutekeleza ibada ya Hijja kwa kila  mwenye uwezo kwani kufanya hivyo ni kutekeleza ibada muhimu na Hijja ni nguzo moja kati ya nguzo tano za Uislamu.

Hayo yameelezwa katika Afisi kuu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar zilizopo Maisara Mjini Unguja na Mwenyekiti wa Al-Ikhlaas Haji,Umra and Travel Agent LT Sheikh Khamis Abdul-Hamid Khamis wakati wa mafunzo maalum ya Ibada ya Hijja kwa wafanyakazi wa Tume hiyo.


Amesema Hijja ni jambo  muhimu kwa kila Muislamu mwenyeuwezo wa hali na mali hivyo wanatoa mafunzo mapema kwasababu kumalizika kwa Ibada ya Hijja hutoa nafasi kwa maandalizi ya Hijja ya mwaka unaofuatia hivyo ni lazima kuwashajihisha waislamu ili kujitaarisha na mapema kufanya ibada Hiyo.

Amesema,waislamu wenye uwezo wa kufanya ibada hiyo ni jambo la lazima na iwapo  wenye uwezo wa fedha na kiafya watashindwa kufanya ibada  hiyo wanakwenda kinyume na kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w) ambae amewahimiza waislamu kwenda kufanya ibada ya Hijja kila mwenye uwezo,

 

Sambamba na hilo ameeleza kuwa,nchi ya Tanzania imepewa nafasi ya kupeleka mahujjaj ishirini na tano elfu (25,000) na Serikali ya Kiislamu ya Saudi Arabia licha ya kupewa nafasi hiyo idadi ya Mahujjaj bado imekuwa ni ndogo kila mwaka kiasi cha kutozidi Mahujjaj elfu nne (4,000) kwa mwaka,vilevile,Serikali ya Saudi Arabia  imetoa tangazo la kufupisha muda wa kuomba maombi ya kufanya ibada Hijja hadi mwezi wa Rajab hivyo kila mwenye nia ya kufanya ibada hiyo kwa mwaka huu ni lazima alipie taratibu zote mapema,hivyo mafunzo hayo yanalenga kuwainua watu,na kuwashajihisha waone umuhimu wa kufanya ibada hiyo. 

Hata hivyo alisisitiza kuwa,kila muislamu anawajibu wa kufanya hijja japo mara moja ndani ya umri wake iwapo amejaliwa kuwa na vigezo vinavyostahiki ikiwemo uwezo, afya na mali.

Aidha amezishajihisha taasisi nyengine za Serikali kuwashajihisha wafanyakazi kwa kuwapatia mafunzo kama haya ili kuwazindua na kila mfanyakazi mwenye uwezo aweze kwenda Hijja mapema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndugu,Thabit Idarous Faina ameishukuru Taasisi ya Al-Ikhlaas Haji,Umra and Travell Agent LTD kwa kuja kushirikiana na wafanyakazi na kuwapatia mafunzo hayo juu ya namna ya kutekeleza ibada ya Hijja kwani licha ya majukumu ya kikazi bado suala la imani litabaki kuwa ni jambo la msingi,wakati akiyasema hayo,

Mkurugenzi Faina,amesisitiza Hijja ni Ibada inayohitaji uwezo hivyo kila mwenye uwezo aone ipo haja ya kufanya ibada hiyo.

Ibada ya Hijja ni nguzo ya tano ya Uislamu na ni ibada yenye historia ya muda mrefu na ilianza kwa nabii wa kwanza katika Uislamu Ibrahim na Ismail,katika zama za Mtume Muhammad (s.a.w) ibada hiyo ilifaradhishwa mwezi wa Dhil-Qaddah, (mwezi wa 11 wa kalenda ya Kiislamu) ya mwaka wa 10 H.A. na hapo ndipo Mtume alitangaza kwamba atatembelea Makka kufanya Hijja.

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii