Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imewataka mawakala ambao watashiriki katika zoezi la uhakiki  na uwandikishaji wa daftari la wapiga kura kutumia vizuri nafasi yao katika  kuelimisha wananchi wenye sifa  kujitokeza  kwa wingi katika vituo vya kuandikisha ili waweze kujiandikisha na  kuhakiki tarifa zao.

Wito huwo umetolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Wete Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Omar Zuber  Mbwana wakati akifungua mafunzo elekezi  kwa mawakala wa uandikishaji  huko katika ukumbi wa skuli ya Sekondari Chasasa Wilaya ya Wete.

Ndugu Omar amesema iwapo mawakala  hao watafuata  taratibu za mafunzo waliyopatiwa kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi na Kanuni za Uandikishaji itasaidia kuwapatia haki wananchi wenye sifa za kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Kwa upande wake , Mkuu wa Kurugenzi ya elimu ya wapiga kura, habari na uhusiano, Juma Sadifu Sheha, amesema mwananchi ambaye atapingwa na mkuu wa kituo cha uandikishaji atapaswa kuchukua fomu  maalumu kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi Nam. 4 ya mwaka 2018, ili kuwasilisha malalamiko yake kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya husika.

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Afisa Uchaguzi Wilaya ya Wete ISSA JUMA HAMADI amewasisitiza mawakala hao kwamba Tume ya Uchaguzi katika zoezi hili la uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura itatumia kitambulisho kipya cha Mzanzibar Mkaazi kilichotolewa na Wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar.

Kwa upande wao washriki  wa mafunzo hayo, Wameishukuru Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuandaa utaratibu mzuri wa Uandikishaji na kuwaomba wananchi kuitumia fursa ya kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

 

Mawasiliano Yetu


Tume ya Uchaguzi Zanzibar

S.L.P 1001 - Zanzibar, Tanzania.

Simu: +255 242231489

Nukushi: +255 242233828

Mitandao ya Kijamii